Jay Z na Beyonce wanatajwa kuwa Couple yenye ushawishi mkubwa na hilo halina ubishi, Huku wakiendelea kushikilia rekodi hiyo wakali hao wa ngoma kama Drunk In Love wametengeneza historia nyingine kwenye maisha yao,

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes takwimu za haraka zinaonyesha utajiri wa Malkia Bey unatajwa kufikia dola milioni 350 na mumewe Jay Z akitajwa Ontop kwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Dola milioni 810 za kimarekani takwimu inayowafanya Jay Z na Bey kuwa na utajiri wa zaidi ya Dola Bilioni 1.6.

Sehemu kubwa ya utajiri wake Jay Z unatokana na harakati (Biashara) zake ikiwemo mtandao wa Tidal ambao umekua ukikua kwa kasi.

Utashanga nikikuambia pamoja na kuwa na mkwanja mrefu kiasi hicho bado Jay Z na Beyonce hawajakua na mamlaka ya kuwa Couple yenye mkwanja mrefu duniani, Cheki na hii Top Ten.

10. Will Smith & Jada Pinkett Smith

Waigizaji maarufu Will Smith na mke wake Jada Pinkett Smith walioudumu kwenye ndoa yao kwa miaka 20 sasa wanatajwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 280.

9. Kanye West & Kim Kardashian

Kanye West alioana na Kim Kardashian May 24 mwaka 2014 mpaka sasa wamejaliwa kuwa na watoto wawili North & Saint. Couple hii kwa sasa  inatajwa kuwa na mkwanja unaokadiriwa kufikia zaidi ya Dola milioni 285

8. Brad Pitt & Angelina Jolie

Utajiri wa waigizaji hawa ulikua uantajwa kufikia Dola milioni 400 kabla ya kutengana kwao mapema mwaka Jana (2016).

7. Tom Brady & Gisele Bundchen

Mwanamichezo Tom Brady na mke wake Gisele Bundchen (Mwanamitindo wa kimataifa) wanamiliki utajiri unaofikia milioni 540.


6. David & Victoria Beckham

Inatajwa kama Couple yenye ushawishi pia hasa kwa nchi za Ulaya, Wanandoa hawa wanatjwa kuwa na utajiri unaofikia Dola milioni 900.

5. Jay-Z & Beyonce

Jay Z na Beyonce wanachukua nafasi ya tano miongoni mwa zile couple zenye mkwanja wa maana, Utajiri wao The Carter family umefikia Dola Billioni 1.6 mwaka huu. (2017)

4. Janet Jackson & Wissam Al Mana

Nafasi ya nne imemilikiwa na Dada wa marehemu Michael Jackson, Janeth Jackson na mumewe bilionea Wissam Al Mana ambao kabla ya kutengana kwao mapema mwaka huu walijaliwa kupata mtot wa kike huku utajiri wao ukitajwa kufikia dola bilioni 1.7

3. Steven Spielberg & Kate Capshaw

Steven Spielberg ni moja kati ya waongozaji maarufu wa filamu (Director) pande za HollyWood yeye na mke wake Muigizaji Kate Capshaw wanatajwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 3.5.

2. Mariah Carey & James Packer

James Packer aliwahi kuripotiwa kumuomba Mariah Carey akubali ombi lake la kuoana kwa pete ya gharama zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya Hollywood Lakini hiyo haikuwa sababu ya kudumisha mahusiano yao, Mpaka wanamwagana Mariah Carey na James walikuwa na jumla ya utajiri uliofikia dola Bilioni 4.2

1. Francois-Henri Pinault & Salma Hayek

Mjasiriamali Bilionea Francois-Henri na mke wake Salma Hayek wapo kwenye ndoa yao tangu mwaka 2009, Raia hao wa Ufaransa wanatajwa kuwa na utajiri unaofikia dola bilioni 5.1 kitu kinachowafanya kuwa Couple yenye mkwanja mrefu zaidi duniani.