Jarida la Forbes limetangaza orodha ya wanamichezo walioingiza mkwanja mrefu kwa mwaka huu na kwa mara nyingine tena Cristiano Ronaldo anaendelea kuishika nafasi ya kwanza.

Kwa mujibu wa Forbes, CR7 anatajwa kufikia utajiri wa dola milioni 93 kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita, Dola milioni 58 Cristiano amevuna kupitia mishahara huku dola milioni 35 akizitengeneza kupitia vitega uchumi vyake.

Mcheza mpira wa Kikapu Lebron James anakua mwanamichezo wa pili alieingiza mkwanja mrefu mwaka huu baada ya kumpiga chini Muajentina Lionel Messi kwa tofauti ya dola milioni 86 kwa 80.

CHEKI NA ORODHA KAMILI HAPA: