Huenda ni kitu ambacho hakikuwa kwenye mawazo yao wakati wa uandaji wa wimbo “Show Me”,habari njema zaidi kwa Harmonize na Rich Mavoko ni hii taarifa iliyotolewa na kituo cha Redio Citizen ya Kenya kupitia kipindi cha “MSETOEA” ambacho hupiga muziki wa Afrika Mashariki, Takwimu zinaonyesha “Show Me” ya washikaji hao wanaowakilisha WCB Wsafi ndio ngoma inayobamba kona zote za Afrika Mashariki.

Licha ya kuwepo kwa vuguvugu la ngoma kali zinazoachiwa kila siku utagundua “Show Me” imeweza kufurukuta kwa kuendelea kufanya vizuri kupitia Vituo mbalimbali vya redio, Mitaani na kwenye vyombo vya usafiri hususan Bajaj na Bodaboda.

Video imeendelea kufanya vizuri  kwenye mtandao wa Youtube  tangu ilipoachiwa April 16 mwaka huu, Mpaka sasa imekwishatazamwa zaidi ya mara milioni 2.

Enjoy Nayo Hapa: