Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anachunguzwa tena baada ya kuvuja kwa idadi kubwa ya barua pepe, zinazodai kugundua mtandao wa rushwa kati yake na familia ya Guptas yenye ushawishi kibiashara.

Nyaraka hizo ambazo zimechapishwa kwenye magazeti ya Afrika kusini, zimedokeza kuwa familia ya Guta ilipokea malipo ambayo yangeweza kuvuka kiwango cha zaidi ya dola milioni 400, katika mpango wa kununua kichwa cha treni kutoka China kwa ajili ya Shirika la Reli la nchi hiyo.

Nyaraka hizo zinadai kwamba familia ya Gupta wangepata dola laki saba na nusu.

Hata hivyo familia ya Gupta bado hawajazungumza chochote kuhusiana na shutuma hizo.