Man Kaur, mwanariadha mwenye umri wa miaka 101 alishinda mbio za mita 100 wakati wa mbio za World Masters Games mjini Auckland, ambapo alisherehekea kwa kucheza densi kidogo.
Bi Kaur alimaliza mbio hizo kwa muda wa dakika moja na sekunde 14 na ndiye mwanariadha pekee kumaliza mbio hizo katika kitengo chake.
Ametajwa kama muujiza kutoka Chandigarh kwenye vyombo vya New Zealand.
Aliruhusiwa kukimbia baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya
Alianza kukimbia akiwa na umri wa miaka 93 akiwa na mtoto wake wa kiume, Gurdev.