Dodoma. Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ameitaka Serikali kuwahoji marais wastaafu ili kufahamu ushiriki wao kwenye sakata la mikataba ya madini.

Amesema kwa ripoti za kamati zilizoundwa na Rais John Magufuli, haiwezekani mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha hilo bila ushiriki wa wakuu wao wa nchi. “Kinga ya marais wastaafu iondolewe na wahojiwe juu ya ushiriki wao kwenye mikataba hii mibovu,” amesema Heche.

Licha ya mpango wa kuzifanyia mabadiliko sheria na sera za madini, Heche ameitaka Serikali kuendeleza mchakato wa katiba mpya pia.