Korea Kaskazinia imeiambia BBC kuwa waziri wake wa mambo ya nchi za kigeni alizungumza na mwenzake wa Korea Kaskazini siku ya Jumapili katika mkutano usio wa kawaida wa uso kwa uso.

Mkutano huo kati ya Kang Kyung-wha wa Korea Kaskazini na Ri Yong Ho ulifanyika pembezoni mwa mkutano wa usalama wa kanda huko Manila.

Msukosuko umeshuhudiwa katika rasi ya Korea miezi ya hivi karibuni huku majaribio kadha ya makombora yakifanywa na Korea Kaskazini.

Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili lilipiga kura kuwekea Korea Kaskazni vikwazo zaidi.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini viliripoti kuwa Bi Kang alisalimiana kwa mkono na bwana Ri wakati wa mkutano mfupi ulioandaliwa na nchi za Asean.