Tume huru ya Uchaguzi nchini Kenya jana Ijumaa Agosti 11, 2017 imemtangaza rais Uhuru Kenyatta kama mshindi wa kiti cha urais.

Viongozi mbalimbali wamemtumia salaam za pongezi akiwemo Dkt. JPM.

Wengine waliomtumia Rasi Kenyatta salaam za pongezi ni Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa, Paul Kagame, Yoweri Museveni na wengine wengi.

Rais Uhuru Kenyatta anakua ameshinda kulihudumia taifa hilo kwa muhula wa pili akitoka kimasomaso kwa ushindi wa kura 8,203,290 (54.27%) .