Mahakama ya Afrika ya Haki za Kibinadamu mjini Arusha Tanzania imeamua kuwaruhusu watu wa kabila la Ogiek nchini Kenya – mojawapo ya makabila madogo sana ya Kiasili nchini humo kurudi katika ardhi waliokuwa wanaishi msitu wa Mau.
Jamii hiyo iliwasilisha kesi dhidi ya serikali ya Kenya katika jitihada za kuruhusiwa kuendelea kumiliki ardhi yao na rasilmali zao.
Mahakama hiyo ya haki za binaadamu sasa imeamua kuwa serikali ya Kenya haikupaswa kuitimua jamii hiyo ya Ogiek kutoka msitu wa Mau kwasababu ardhi hiyo ni yao ya jadi.
Rashamba Debola, wa kabila la Ogiek anasema “nilizaliwa katika msitu wa Mau, nikaolewa hapa kitamaduni, nikazaa hapa, na nikamzika mume wangu katika msitu huu.”