Aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kufanya kazi kwenye baraza kuu la wakimbizi duniani WRC, ambalo ni kundi huru la viongozi na wavumbuzi wanaolenga kubuni mbinu mpya za kutatua mizozo ya wakimbizi.

Kulingana na gazeti la The Citizen taarifa kwa vyombo vya habari ilimtaja Jakaya Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza wa baraza hilo lililopo chini ya uenyekiti wa waziri wa mambo ya Nje wa Canada Lloyd Axworthy.

Gazeti hilo limesema kuwa Hina Jinali kutoka Pakistan na Rita Sussmith kutoka Ujerumani watafanya kazi pamoja  Kikwete kama wenyekiti wenza huku Paul Heinbecker akichaguliwa kama naibu huku naye Fen Hamson akihudumu kama mkurugenzi.

Taarifa hiyo imesema kuwa miongoni mwa mengine, baraza hilo litatoa ushauri wa marekebisho na uvumbuzi ili kuimarisha mfumo wa wakimbizi wote  duniani.