Tuzo za muziki za Billboard kwa mwaka huu 2017 zimefanyika usiku wa jana May 21,2017 kwenye ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas,

Moja kati ya kilichoonekana kuwa kivutio zaidi kwa Nigeria na Afrika ni ushindi wa StarBoy Wizkid ambae alifanikiwa kuondoka na jumla ya Tuzo 4 kupitia wimbo “One Dance” na kuitengeneza historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza Afrika kushinda Tuzo hizo tangu kuanzishwakwake mwaka 1990.