Kundi moja la kina mama mjini Dar es Salaam, wakiwemo wajane na waathrika wa Virusi vya Ukimwi, wameungana na kubuni njia ya kuvutia ya kupata riziki kupitia utengenezaji wa vyakula vya mifugo kwa kutumia damu ya ng’ombe.

Kina mama hao wameanzisha biashara hiyo kujikimu kimaisha na kujitegemea licha ya changamoto wanazopitia.

Kwenye hii taarifa iliyotolewa na Shirika la utangazaji la BBC wanasikika kinamama hao wakielezea mipango yao.