Klabu ya soka ya Chelsea imefuta ziara ya kulitembeza kombe la EPL mjini Manchester baada ya shambulizi la siku ya Jumapili kwenye tamasha la mwanamuziki Ariana Grande.

Klabu hiyo imesema kuwa haitakuwa jambo jema kuwafanya watu warundikane kwa wakati huu ambao ulinzi umeimarishwa mjini Manchester.

Chelsea imepanga kutumia basi la wazi kulitembeza kombe hilo Uingereza na iwapo watafanikiwa kushinda la FA dhidi ya Arsenal siku ya Jumamosi watajumuisha yote.

Wachezaji wa Chelsea kwa pamoja watatoa michango yao kwa wahanga.

Pia watavaa vitambaa vyeusi siku ya mchezo wa fainali ya FA Jumamosi watakapochuana na Arsenal.